Saturday, August 11, 2012

KIOO CHETU




        Jukumu la kutunza maadili ya mzanzibar si la serikali pekee ni la kila mtu kuzingatia utamaduni na sirika za kijamii hivyo basi ili maadili yetu yawe kioo katika anga za kimataifa ni muhimu kuenzi mambo ya msingi yanayoendana na uhalisia wa maisha yetu ya kila siku,si vyema kujifunza tamaduni za kigeni ambazo haziendani na asili zetu.

Katika makala hii mwandishi ataangazia katika nyanja ya lugha yetu nzuri ya kiswahili si jambo la ajabu kuwaona viongozi mbalimbali wanapokuwa wakishiriki katika majukwaa ya kimataifa kwa lengo la kuwawakilisha wananchi wao hawana utamaduni wa kutumia lugha ya taifa lao suala linalopelekea kutokuwepo na misingi imara ya kutangaza lugha ya kiswahili kama nembo ya taifa.

No comments:

Post a Comment